Posts

Showing posts from January, 2024

SHULE YA UPILI YA KAYA TIWI YAFUNGWA.

Image
SHULE YA UPILI YA KAYA TIWI YAFUNGWA. Shule ya upili ya Kaya Tiwi katika kaunti ya Kwale imefungwa kwa muda, baada ya wanafunzi kuzua rabsha katika shule hiyo mapema leo asubuhi, wakidaiwa kuzua vurugu hizo wakipinga uhamisho wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Chigamba Chilembi.

Samaki wa Ziwa Nakuru wapigwa marufuku.

Image
MVURYA APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA SAMAKI WA ZIWA NAKURU. Samaki wanaovuliwa kutoka Ziwa Nakuru hawafai kwa matumizi ya binadamu, hili ni Onyo la Waziri wa Madini, Uchumi samawati na Masuala ya Baharini Salim Mvurya. Akizungumza katika Kaunti ya Embu siku ya Jumatano 24 Januari baada ya kufanya mazungumzo na Gavana wa kaunti hiyo Cecile Mbarire, Mvurya alisisitiza kwamba majaribio ya hivi majuzi yaliyofanywa yalibaini kuwa samaki wanaopatikana kutoka Ziwa Nakuru walionyesha kuwa na kiwango cha juu cha arsenic, kemikali inayopatikana katika madini mengi Ulimwenguni. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), matumizi ya muda mrefu ya kemikali ya arseniki kupitia unywaji wa maji na vyakula unaweza kusababisha saratani na vidonda vya ngozi. Zaidi ya hayo, kemikali hii ilihusishwa na ugonjwa wa moyo na mishipa pamoja na ugonjwa wa kisukari. Dalili za moja kwa moja za sumu ya arseniki ni pamoja na kichefuchefu, kutapika na kuhara.

maradhi ya macho mombasa(red eye)

Image
MARADHI YA MACHO YAENDELEA KUWATATIZA WAKAAZI WA KAUNTI YA MOMBASA.(RED EYE) Zaidi ya watu elfu moja kaunti ya Mombasa wanaugua maradhi ya macho mekundu yaliyoripotiwa kuzuka katika kaunti hii. Idara ya Afya kaunti ya Mombasa imethibitisa hilo huku ikibaini kuwa idadi hiyo huenda ikawa ni kubwa zaidi kutokana na baadhi kuwa hawajafika katika vituo vya afya. Idara hio iliendelea kutoa tahadhari kwa wakaazi wote na hasa wazazi kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo. Kulingana na Afisa wa Afya kaunti ya Mombasa Abdallah Deleno, watoto na watu wazima ni miongoni mwa waathiriwa. Deleno aliwataka wakazi kutokuwa na hofu akiyataja maradhi hayo kuwa ya kawaida japo akitoa himiza ya kuchukua tahadhari ili kujilinda na maradhi hayo ikiwemo kudumisha usafi kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni na kujizuia kushika macho kila mara. by:RUKIA AMIN

siku ya kawi ulimwenguni.

Image
SIKU YA KIMATAIFA YA KAWI SAFI:  Kenya  imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nishati Safi hii leo. Siku hiyo huadhimishwa kila tarehe 26 Januari kila mwaka kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni mfumo endelevu wa nishati safi katika siku za usoni yaani (“Clean Energy: The transition to a sustainable future”.) Katika kaunti ya Mombasa maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Bustani ya Uhuru, eneo la Mapembeni hadi eneo la Treasury Square ambako kilele cha maadhmisho hayo yalifanyika kwa maonyesho mbalimbali na hotuba za viongozi. Waziri wa uchukuzi kaunti ya Mombasa Daniel Manyara amesema wizara yake inafanya mazungumzo kuhakikisha kuwepo na utumizi wa nishati safi kwenye sekta ya usafiri. by: RUKIA AMIN