Samaki wa Ziwa Nakuru wapigwa marufuku.
MVURYA APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA SAMAKI WA ZIWA NAKURU.
Samaki wanaovuliwa kutoka Ziwa Nakuru hawafai kwa matumizi ya binadamu, hili ni Onyo la Waziri wa Madini, Uchumi samawati na Masuala ya Baharini Salim Mvurya.
Akizungumza katika Kaunti ya Embu siku ya Jumatano 24 Januari baada ya kufanya mazungumzo na Gavana wa kaunti hiyo Cecile Mbarire, Mvurya alisisitiza kwamba majaribio ya hivi majuzi yaliyofanywa yalibaini kuwa samaki wanaopatikana kutoka Ziwa Nakuru walionyesha kuwa na kiwango cha juu cha arsenic, kemikali inayopatikana katika madini mengi Ulimwenguni.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), matumizi ya muda mrefu ya kemikali ya arseniki kupitia unywaji wa maji na vyakula unaweza kusababisha saratani na vidonda vya ngozi.
Zaidi ya hayo, kemikali hii ilihusishwa na ugonjwa wa moyo na mishipa pamoja na ugonjwa wa kisukari. Dalili za moja kwa moja za sumu ya arseniki ni pamoja na kichefuchefu, kutapika na kuhara.
Comments
Post a Comment