siku ya kawi ulimwenguni.
SIKU YA KIMATAIFA YA KAWI SAFI:
Kenya imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nishati Safi hii leo.
Siku hiyo huadhimishwa kila tarehe 26 Januari kila mwaka kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni mfumo endelevu wa nishati safi katika siku za usoni yaani (“Clean Energy: The transition to a sustainable future”.)
Katika kaunti ya Mombasa maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Bustani ya Uhuru, eneo la Mapembeni hadi eneo la Treasury Square ambako kilele cha maadhmisho hayo yalifanyika kwa maonyesho mbalimbali na hotuba za viongozi.
Waziri wa uchukuzi kaunti ya Mombasa Daniel Manyara amesema wizara yake inafanya mazungumzo kuhakikisha kuwepo na utumizi wa nishati safi kwenye sekta ya usafiri.
by: RUKIA AMIN
Comments
Post a Comment