UDHIBITI WA MASAROVEA BANDIA NCHINI
Erick nyadimo (middle) Rais wa Taasisi ya Masoroveya nchini, ISK, Erick Nyadimo ametoa wito kwa serikali kutenga fedha za kutosha kwa Bodi ya Kudhibiti Masoroveya ili kusaidia juhudi za kukabiliana na ongezeko la masoroveya bandia nchini. Akizungumza mjini Mombasa wakati wa kongamano lililowaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta hiyo, Nyadimo amesema kuwa uwezeshaji wa kifedha pamoja na upatikanaji wa rasilimali za kutosha kwa bodi hiyo utachangia kuimarisha usimamizi wa taaluma na kudhibiti uwepo wa masoroveya bandia. Aidha, amesema kuwa marekebisho ya kisheria katika uendeshaji wa sekta hiyo yatasaidia kwa kiwango kikubwa kukabiliana na changamoto hiyo. Vilevile, amesisitiza umuhimu wa kuangazia masomo ya muda mfupi katika taaluma ya usoroveya ili kuwapa wanafunzi muda na nafasi ya kutosha kukuza uwezo wao kitaaluma, hatua ambayo pia itasaidia kupunguza idadi ya wataalamu bandia katika sekta hiyo.